1 Corinthians 14:1-6

Karama Za Unabii Na Lugha

1 aFuateni upendo na kutaka sana karama za roho, hasa karama ya unabii. 2 bKwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho. 3 cLakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji. 4 dAnenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa. 5 eNingependa kila mmoja wenu anene kwa lugha lakini ningependa zaidi nyote mtoe unabii. Kwa kuwa yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, isipokuwa atafsiri, ili kanisa lipate kujengwa.

6 fSasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?
Copyright information for SwhKC